Watu 412 zaidi wapona corona wengine wanne wakifariki

0

Watu wengine 123 wamekutwa na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 4,948 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 98,555 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia 81,667 baada ya watu 412 kupona.

Wagonjwa wanne zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 1,720.

Wagonjwa waliolazwa hospitalini ni 675 huku 1,945 wakishughulikiwa nyumbani. Waliolazwa katika chumba cha watu mahututi (ICU) ni 26.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here