Watu 1,459 zaidi wamekutwa na virusi vyua COVID 19 baada ya kupima sampuli 10,146 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 74,145.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kupona kwa watu 780 na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 50,658.
Aidha idadi ya maafa imeongezeka baada ya watu 17 kufariki kutokana na makali ya ugongwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 1,330.
Kufikia sasa wagonjwa 1,116 wamelazwa katika hospitali mbalimali na 6,232 wakihudumiwa nyumbani.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifyatavyo; Nairobi inaogoza kwa kuripoti visa 472, Kiambu 311, Mombasa 108 na Laikipia 63.









