Magoha alikosea kufunga shule, mahakama yaamuru

0

Mahakama imeamuru kuwa ilikuwa makosa kwa waziri wa elimu Profesa George Magoha kufunga shule hadi mwaka ujao pasipo kushauriana na wazazi.

Akitoa uamuzi huo, jaji wa mahakama kuu James Makau ameamuru kuwa uamuzi huo ulikiuka haki msingi za wanafunzi licha ya kwamba taifa linakabiliwa na janga la corona.

Na sasa jaji Makau ameagiza kufunguliwa kwa shule chini ya siku sitini zijazo kuanzia leo.

Kesi hiyo ya kupinga kufungwa kwa shule iliwasilishwa mahakamani na mkenya Joseph Enock aliyehoji kuwa wizara ya elimu ina uwezo wa kuweka mikakati inayofaa na kuwaacha wanafunzi kuendelea na masomo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here