Maaskofu wa kanisa katoliki wameelezea wasiwasi wao kuhusu idadi ya wahudumu wa afya wanaopoteza maisha kutokana na virusi vya corona.
Katika taarifa, maaskofu hao wameilaumu serikali na wanaitaka kulipa kipau mbele swala la kuwakinga wahudumu wa afya dhidi ya kuambukizwa virusi hivyo.
Aidha, viongozi hao wa kidini wamejiunga na madaktari kutoa wito kwa serikali kutenga fedha zaidi ili kuboresha sekta ya afya nchini.
Na ili kuepuka mgomo wa madaktari unaonukia, maaskofu hao wanaitaka serikali kuitisha mazungumzo yenye lengo la kutanzua mgomo huo.
Kufikia sasa, wizara ya afya inasema wahudumu wa afya waliofariki kutokana na ugonjwa huo ni 30 maelfu ya wengine wakiwa wameambukizwa virusi hivyo.