Mwanafunzi mwingine ashikwa na kisu shuleni Kwale

0

Makachero wa idara ya upelelezi DCI huko Kwale wameshika mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 kwa kupatikana na kisu darasani.

Mwanafunzi huyo amekamatwa baada ya mwalimu mkuu Salah Yeri kuripoti kuwa baadhi ya wanafunzi walikuwa wameingia darasani wakiwa na visu.

Uzuri ni kwamba hamna aliyejeruhiwa kwani Polisi walifaulu kufanya msako na kupatika kisu hicho.

Haya yanajiri huku wanafunzi wawili katika kaunti za Kisii na Nyamira wakishikwa kwa kuwashambulia walimu wao kwa kutumia silaha.

Tume ya huduma za walimu TSC imelaani vikali utundu huo wa wanafuzni kuwavamia walimu wao na kuomba wazazi na walezi kuwapa ushauri nasaha wanao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here