Naibu Gavana mteule Nairobi Ann Mwenda ahojiwa

0

Ann Kananu Mwenda ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na shirika la NMS iwapo ataidhinishwa kuwa naibu Gavana, na kisha kuapishwa kuwa Gavana wa kaunti ya Nairobi.

Akihojiwa na kamati maalum ya bunge la kaunti ya Nairobi ikiongozwa na kiongozi wa wengi Abdi Guyo, Kananu amesema ushirikiano baina ya serikali ya kaunti na NMS ndio ambao utachangia maendeleo jijini.

Mwenda amesema ana ufahamu kwamba ‘makateli’ wamekuwa changamoto jijini Nairobi na kuahidi kufanya kila awezalo kupambana na kundi hilo la wahuni na pia kusuluhisha baadhi ya matatatizo ya kaunti ikiwemo mrundiko wa taka na msongamano wa magari.

Alipofika, Mwenda alitakiwa mwanzo kuelezea anachokifahamu kuhusu ugatuzi.

Kamati hiyo kwa sasa inatengeneza ripoti ambayo watawasilisha kwa bunge la kaunti ambalo litaidhinisha au kukatalia mbali uteuzi huo uliofanywa na aliyekuwa Gavana Mike Sonko Januari mwaka uliopita.

Kananu ambaye kwa sasa ni afisa wa majanga katika kaunti ya Nairobi aliteuliwa Januari mwaka uliopita lakini mkaaji mmoja akaelekea mahakamnai kupinga uteuzi wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here