Mwanafunzi aliyekosa karo asaidiwa

0

Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua ameingilia kati na kumsaidia Philomena Mutheu, mtahiniwa wa kidato cha nne aliyekuwa amefukuzwa shuleni kwa kukosa karo.

Mutheu mwenye umri wa miaka kumi na saba katika shule ya St.Mary’s Kithangaini alivutia hisia kutoka kwa Wakenya kupitia kwa barua aliyokuwa amemuandikia rais Uhuru Kenyatta akimfahamisha kwamba yeye ni yatima na anapitia matatizo mengi yaliyohitaji msaada.

Hata hivyo Dkt. Mutua katika taarifa amesema amemlipia mwanafunzi huyo karo aliyokuwa anadaiwa ya Sh26,958 ili kumuwezesha kurejea shuleni.

Gavana Mutua ameitaka serikali kutekeleza ahadi yake kwamba mwanafunzi yeyote asifukuzwe shule kwa kukosa karo wakati huu wa corona.   

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here