Afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya Mama Lucy Emma Mutio ni miongoni mwa washukiwa watatu waliokamatwa kuhusiana na sakata ya wizi wa watoto wachanga kufuatia ufichuzi wa shirika la habari la BBC.
Wengine ni msimamizi wa hospitali hiyo Regina Musembi na mfanyikazi wa hospitali hiyo Fred Leparan.
Watatu hao watazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Kilimani hadi Alhamisi wakisubiri hatma yao mahakamani.
Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai anasema watatu hao ni miongoni mwa genge ambalo limekuwa likiwaiba watoto kabla ya kuwauza kwa kati ya shilingi Sh70,000 hadi Sh300,000.
Mutyambai anasema vituo vya watoto mayatima ama kutoka familia ambazo hazijiwezi na baadhi ya hospitali za umma kaunti ya Nairobi vinahusika kwenye sakata hiyo.