Huduma Namba kuchukua nafasi ya vitambulisho vya kitaifa yasema serikali

0

Kufikia tarehe 12 Disemba mwaka ujao wa 2021, Wakenya hawatatumia tena vitambulisho vya kitaifa.

Badala yake, waziri wa ICT Joe Mucheru anasema kadi za Huduma Namba ndizo ambazo zitatumika kama vitambulisho.

Akizungumza alipozindua zoezi la usambazaji wa kadi hizo katika kaunti ya Machakos, Mucheru amesema wakenya wataanza kupokea kadi za Huduma kuanzia tarehe moja Disemba mwaka huu.

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i ameongoza uzinduzi wa kadi hiyo ya Huduma Namba katika kaunti ya Kiambu.

Wakenya watafahamishwa kuhusu watakavyopata kadi zao kupitia ujumbe utakaotumwa kwenye simu zao.

Usajili mwingine wa Wakenya kupata Huduma Namba utaanza Aprili 21 mwaka ujao, 2021.

Kadi hizo zitatolewa kwa watoto waliotimu umri wa miaka sita, watu wazima waliofikisha umri wa miaka kumi na nane, raia wa kigeni na kwa wakimbizi ambao pia watapewa kadi zao. 

Mchakato huo umeanza baada ya kuapishwa kwa Immaculate Kassait kama kamishna wa Data.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here