Watu 2,616 zaidi wamepona kutokana na virusi vya covid 19 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 49,878.
Miongoni mwa waliopona ni wagonjwa 2,434 waliokuwa wakihudumiwa nyumbani huku wengine 182 wakitibiwa katika hospitali mbalimbali.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibibitisha kuwa wagonjwa wengine 11 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,313.
Aidha watu wengine 957 wamedhibitishwa kuambukizwa virusi hivyo na kufikisha idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kuwa 72,686.
Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa idadi ya maambukizi kwa kurekodi visa 368, Nyeri 53, Kitui 41 na Kiambu 40.
Kufikia sasa wagonjwa 1,191 wanahudumiwa katika hospitali mbalimbali wengine wengine 6,000 wakishughulikiwa nyumbani.
Wahudumu wa afya walioambukizwa virusi hivyo ni 2,369 huku 30 wakiwa wamefariki.