Mvua kubwa zinazoshuhudiwa katika sehemu mbalimbali nchini zinatazamiwa kupungua Ijumaa na Jumamosi imesema idara ya utabiri wa hali ya anga.
Idara hiyo inazidi kutoa tahadhari kwa kila mmoja kuwa makini kwa sababu mvua hizo zinasababisha mafuriko ambayo huenda yakasababisha maafa.
Mvua hizo zinatazamiwa kupungua katika maeneo ya Rift Valley pamoja na Nairobi.
Familia nyingi zimebaki bila makao tangu kuanza kwa mvua hizo baada ya makaazi yao kusombwa na maji.









