Bei ya Petroli yapanda kwenye bei mpya za EPRA

0

Bei za mafuta taa pamoja na Diseli zitasalia zilivyo kwa muda wa mwezi mmoja ujao huku mafuta ya Petroli yakiongezwa kwa Sh3.56.

Hii ni kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa Ijumaa na tume ya kudhibiti kawi nchini EPRA.

Lita moja ya Petroli jijini Nairobi itauzwa kwa Sh126.37, mjini Mombasa itauzwa kwa Sh123.96, mjini Nakuru itapatikana kwa Sh125.98 huku wakaazi wa Eldoret na Kisumu wakinunua kwa Sh126.90.

Wakaazi wa Nairobi wataendelea kununua mafuta taa kwa Sh97.85, Mombasa Sh95.46, Nakuru Sh97.76, Eldoret na Kisumu Sh98.68.

Lita moja ya Diseli itaendelea kuuzwa Sh107.66 jijini Nairobi, Sh105.27 jijini Mombasa, Sh107.35 mjini Nakuru na Sh108.46 mjini Eldoret.

Itakumbukwa kwamba bei za bidhaa hiyo zilisalia zilivyokuwa mwezi Machi kufuatia vilio kutoka kwa Wakenya waliolalamikia kusongwa na hali ngumu ya kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here