Hatima ya Gavana Mohamed Mohamud kujulikana Jumatatu

0

Kamati ya maseneta 11 iliyotwikwa jukumu la kuamua hatma ya kung’olewa kwa gavana wa Wajir Mohamed Mohamud Abdi imeenda faraghani kuandika ripoti yake.

Kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Nyamira Okong’o Omogeni inatazamiwa kuwasilisha ripoti yake bungeni Jumatatu ijayo.

Spika wa bunge la Senate Ken Lusaka ameratibu kikao maalum kuandaliwa Jumatatu Mei 17 kutathmini ripoti ya kamati hiyo.

Gavana Mohamed Mohamud Abdi amejitetea vikali dhidi ya madai ya ufisadi pamoja na utumizi mbaya wa afisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here