Kenya haijaripoti maafa yoyote yanayotokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na hivyo kufanya idadi ya maafa kusalia kuwa 577.
Katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Rashid Aman aidha ametangaza kuwa watu 318 zaidi wamepona ugonjwa huo na kuongeza idadi ya waliopona na kufikia 20,211.
Vile vile, visa vipya 114 vya ugonjwa huo vimeripotiwa nchini baada ya kupima sampuli 1,682 na kuongeza idadi ya visa hivyo nchini kuwa 34,315.
Msambao wa virusi hivyo katika kila kaunti ni kama ifwatavyo; Mombasa 17, Nairobi 16, Garissa 15, Kiambu na Kitui 14, Busia 12, Taita taveta 8, Uasingishu 6,Nyeri 5, Embu na Kisumu 1.









