Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya visa vya ugonjwa wa corona kufikia sasa.
Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amesema Nairobi 19,494, ikifuatiwa na Kiambu iliyo na visa 2,524 huku Mombasa ikiwa ya tatu kwa kurekodi visa 2,387.
Kaunti ya Kajiado ya nne kwa kurekodi visa 1,878, Machakos ni ya tano kwa kurekodi visa 1,246 huku Busia ikiandikisha visa 1,087.
Kaunti za Elgeyo Marakwet na West Pokot ndizo zimeandikisha idadi ndogo ya virusi hivyo kwa kuwa na visa 6.