Jaji Njagi Marete kurejeshwa kazini

0

Jaji wa mahakama ya Leba Njagi Marete atarejeshwa kazini baada ya jopo lililobuniwa kumchunguza kumuondolea lawama.

Jopo hilo linaloongozwa na jaji mstaafu Alnashir Visram katika uamuzi wake limebaini kuwa jaji huyo hana hatia yoyote kufuatia madai ya muungano wa wakuzaji wa majani chai kwamba alikiuka maadili ya utendakazi alipotoa uamuzi kwenye kesi yao.

Muungano huo wa wakuzaji wa majani chai ulitaka kuondolewa kwa jaji huyo kwa misingi kwamba alitoa uamuzi kwenye kesi ambayo ilikuwa tayari imeshughulikiwa na jaji mwenzake.

Awali, jaji Njagi alishindwa kwenye kesi ambapo alitaka kuzuia kubuniwa kwa jopo kumchunguza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here