TSC kuwaajiri walimu

0

Tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC imeatangaza nafasi elfu tano za ajira kwa walimu wa shule za upili ili kuongeza idadi ya walimu nchini.

Katika notisi tume hiyo inasema hatua hiyo inalenga kufanikisha mpango wa serikali wa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakalia mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE wanajiunga na shule za upili.

Walimu ambao wamehitimu na wangependa kujaza nafasi hiyo wametakiwa kutuma maombi yao kupitia kwa wavuti wa www.tsc.go.ke.

Wanaotakiwa kutuma maombi yao ni wakenya walio na shahada ya Elimu (Diploma), wawe wamejisajili na tume hiyo, miongoni mwa matakwa mengine.

Iwapo unahitimu na ungependa kutuma maombi yako, una hadi tarehe kumi na nne mwezi huu kutuma maombi yako kwa tume hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here