Matabibu kujiunga na madaktari, wauguzi kwenye mgomo

0

Muungano wa matabibu nchini KUCO umesema utaendelea mbele na mgomo wake kuanzia Jumatatu hii iwapo matakwa yao hayatatekelezwa.

Katibu mkuu wa muungano huo George Gibore amesema kuwa serikali haijashughulikia malalamishi yao ikiwemo kuwapa vifaa vya kujikinga PPEs na hata bima ya matibabu.

Amesema wenzao tisa wamefariki kutokana na corona kufikia sasa huku wengine 763 wakiambukizwa virusi hivyo.

Maafisa hao walitoa ilani ya mgomo ambayo inatazamiwa kukamilika Jumapili ambayo ni December tarehe 6.

Mgomo huo unatazamiwa kuanza sambamba na ule wa madaktari na Wauguzi huku serikali ikiwarai wasisuie kazi mazungumzo yakiendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here