Ushuru uliokuwa umeondolewa kurejeshwa kuanzia Januari

0

Wakenya wanaopata mshahara usiozidi Sh24,000 hawataendelea kutozwa kodi huku serikali ikitangaza kuwa itarejesha ushuru uliokuwa umeondolewa kuwaokoa Wakenya kutokana na makali ya corona kuanzia mwezi ujao.

Waziri wa Fedha Ukur Yattani ametangaza kurejesha ushuru uliokuwa umeondolewa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

Yattani amesema katika kipindi cha miezi saba ambapo ushuru huo ulikuwa umeondolewa, taifa lilipoteza Sh65b.

Hii inamaanisha kuwa kampuni pamoja na wafanyiabashara watatozwa ushuru serikali inapolenga kujikwamua kifedha.

Kwa mfano, ushuru wa asilimia 14% kwa bidhaa yaani VAT uliokuwa umesimishwa utarejeshwa na mara hii bidhaa zitatozwa asilimia 16% ya ushuru.

Ushuru kwa mapato yaani PAYE utaongezwa kutoka asilimia 25% hadi 30%.

Aidha miradi mbalimbali iliyokuwa imeanzishwa kuwalinda Wakenya dhidi ya mahangaiko yanayosababishwa na hali ngumu ya kiuchumi kama vile Kazi Mtaani itaendelea.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here