Tume ya huduma za mahakama (JSC) imefutilia mbali ombi lililokuwa linataka kutimuliwa kwa majaji watatu wa mahakama ya upeo.
JSC katika uamuzi wake imebaini kuwa madai dhidi ya watatu hao Mohamed Ibrahim, Smokin Wanjala na Njoki Ndungu hayana msingi wowote na hayawezi yakadhibitishwa.
Mlalamishi Jared Ongeri alikuwa anadai kuwa majaji hao watatu walishawishiwa na mwanasiasa fulani ili kumpendelea Gavana Mohamed Abdi kwenye uamuzi wao.
Hata hivyo JSC inasema mlalamishi alikosa kuwasilisha ushahidi wa kudhibitisha madai yake dhidi ya watatu hao.