Matiang’i akemea mauaji ya GSU Kapedo

0

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amekemea mauaji anayoyataja kama ya kinyama dhidi ya maafisa wa usalama waliokuwa kwenye zamu katika eneo la Kapedo.

Shambulizi hilo lililotokea katika eneo la Kapedo na Chemolingot kaunti ya Baringo Jumapili jioni lilisababisha kuuawa kwa afisa mmoja wa GSU aliyepia mkurugenzi wa oparesheni Emadau Temako na kuwajeruhi maafisa wengine wawili.

Waziri Matiang’i katika taarifa amefichua kwamba mauaji hayo yalipangwa kwani waliohusika walikuwa wametoka katika sherehe za kitamaduni ambapo walikula kiapo.    

Amesema oparesheni ya kuwatafuta waliohusika imeanzishwa na watakaopatikana wataadhibiwa vikali kisheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here