Mwanafunzi wa darasa la nne amtilia babake sumu kwa uji kwa kupinga uhusiano wake na mtahiniwa wa kidato cha nne

0

Mwanafunzi wa darasa la nne huko Kisii ameshikwa na Polisi kwa madai ya kujaribu kumpa sumu babake kwa kupinga uhusiano wake na mpenziwe ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne.

Mwanafunzi huyo wa shule ya msingi ya Kegati anadaiwa kuchukua sumu na kuitia kwenye uji wa babake baada yake kumuuliza kuhusu uhusiano wake na mvulana mwenye umri wa miaka 19 na mwanafunzi wa shule ya upili ya Kegati.

Majirani wanadai kuwa wanafunzi hao wamekuwa katika mahusiano kwa miezi kadhaa na walipanga njama ya kumuua mzee huyo baada yake kuwakanya dhidi ya mahusiano hayo.

Akidhibitisha kisa hicho, kamanda wa Polisi Kisii Jebel Munene amesema wawili hao watashtakiwa kwa jaribio la mauaji.

Polisi wanasema mwanafunzi huyo alisema ukweli baada ya babake kufahamu kuwa uji wake haukua na harufu ya kawaida.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here