Maafisa wawili wa polisi na mfanyiakzi wa benki wamekamatwa kuhusiana na wizi wa wa pesa kutoka benki ya Prime tawi la barabara ya Mombasa.
Idara ya upelelezi nchini DCI inasema maafisa hao walikuwa kwenye zamu wakati wizi huo ulitekelezwa hapo jana.
DCI inasema maafisa wanachunguzwa kuhusiana na vipi wezi hao walifaulu kuwapokonya bunduki zao na risasi sitini.
Bunduki hizo zilipatikana baadaye nje ya lango la hospitali ya Kiambu.
Kiasi kisichojulikana cha pesa kilipotea wakati wa mkasa huo.