Wanafunzi wawili watoroka shuleni Kitui

0

Maafisa wa polisi wanawasaka wanafunzi wawili kutoka shule moja ya upili kaunti ya Kitui wanaoripotiwa kutoroka shuleni siku ya Ijumaa.

Wawili hao, msichana wa kidato cha pili na mvulana wa kidato cha kwanza wanaripotiwa kutoroka shuleni pamoja bila ufahamu wa walimu na hawakuelekea nyumbani kwao.

Dadake msichana huyo amekiri kuwaona wawili hao wakitoka shuleni pamoja kabla ya kupiga ripoti kwa mamake ambaye aliwafahamisha maafisa wa polisi baada ya juhudi zake kuwatafuta kugonga ukuta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here