JSC yatangaza rasmi nafasi ya jaji mkuu kuwa wazi

0

Je, unamezea mate wadhifa wa jaji mkuu baada ya kustaafu kwa David Maraga?

Sasa basi uko huru kutuma rasmi maombi yako kufuatia kutangazwa kwa nafasi hiyo kuwa wazi na tume ya huduma za mahakama JSC.

Kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu ambaye pia anashikilia wadhifa wa mwenyekiti wa JSC katika gazeti rasmi la serikali amewataka wanaomezea mate kiti hicho kutuma maombi yao kabla ya Februari 10.

Atakayefaulu kuwa jaji mkuu atarajie mshahara wa Sh1.3M mbali na marupurupu mengine.

Watakaotuma maombi yao wametakiwa kuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika idara ya mahakama.

Mahitaji mengine ni kuwa na digrii kwenye taaluma ya uanasheria kutoka chuo chochote kinachotambulika.

Vile vile, unahitajika kuwa na maadili mema kwa kuzingatia sehemu ya Sita ya katiba ya Kenya.

Philomena Mwili atasalia kushikilia wadhifa huo mpaka mrithi wa Maraga apatikane ila haijabainika wazi iwapo atatuma maombi ya kuwania wadhifa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here