Manduku akanusha mashtaka ya ufisadi KPA

0

Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari KPA Daniel Manduku amekanusha mashtaka ya kushirikiana kutekeleza uhalifu wa kiuchumi na mashtaka mengine kadhaa ya utumizi mbaya wa afisi.

 Manduku amefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama za milimani Lawrence Mugambi ambapo pia ameshtakiwa pamoja na afisa wa kpa juma fadhili wote wakikabiliwa na shtaka moja la utumizi mbaya wa afisi na kwa pamoja wakishtakiwa kwa kushirikiana kutekeleza kitendo cha ufisadi.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa kpa alijisalimisha kwa maafisa wa EACC kufuatia madai ya kulipa shilingi milioni mia mbili arobaini nan ne nukta tisa kwa wanakandarasi kwa kazi ambayo hawakuwa wameimalizia.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here