Kamati ya bunge la Seneti kuhusu uhasibu imeamuagiza Inspekta mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai kumkamata gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria na kumleta mbele ya kamati hiyo kujibu maswali kuhusu matumizi ya pesa.
Kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Kisii Sam Ongeri vile vile imempiga gavana huyo faini ya Sh500, 000 kwa kufeli kufika mbele yake mara tatu.
Mutyambai ametakiwa kumfikisha gavana huyo mbele ya kamati hiyo Septembe 10.
Kanuni za bunge zinairuhusu kuagiza kukamatwa kwa yeyote anayekosa kuheshimu wito wa kuitaka kufika mbele yake.