Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameagizwa na mahakama ya Mombasa kufika mbele yake siku ya Jumatatu kujibu mashtaka ya wizi wa sh57M pesa za ustawishaji maeneo bunge CDF.
Hakimu wa Mombasa Edna nyaloti amemwagiza jumwa kufika mbele yake ili kusomewa mashtaka dhidi yake huku pia akitakiwa kujiwasilisha katika kituo cha polisi cha Port ambapo ataweza kuchukuliwa ripoti na stakabadhi kabla ya kuruhusiwa kufika mahakamani.
Hata hivyo washukiwa wengine sita na ambao wanasimamia miradi ya CDF Malindi wamefikishwa mahakamani ambapo wamekanusha mashtaka dhidi yao na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu shilingi milioni tano kila mmoja.