Keziah Onyango, mamake wa kambo aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama amefariki.
Kupitia mtandao wake wa Twitter, mwanawe Auma Obama amedhibitisha kuwa Keziah,81, amefariki akipokea matibabu nchini Uingereza baada ya kuugua.
Wiki mbili zilizopita, familia ya Obama ilimpoteza Mama Sarah Obama ambaye alizikwa nyumbani kwake Kogelo kwenye hafla fupi iliyohudhuriwa na ndugu wa karibu.