Mahakama ya Runyenjes imefungwa kwa muda wa siku saba baada ya wafanyikazi nane kupatikana na ugonjwa wa corona.
Kulingana na kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu, mahakama hiyo imefungwa ili kutoa nafasi kwa wafanyikazi zaidi kupimwa iwapo wana ugonjwa huo.
Mwilu amesema kesi za dharura kwenye mahakama hiyo sasa zitashughulikiwa na mahakama za Embu na Kerugoya.
Haya yanajiri huku idadi ya maambukizi ya nchini yakifikia 147,147.