Mahojiano ya kumsaka jaji mkuu mpya yaingia siku ya tatu

0

Mahojiano ya kumtafuta jaji mkuu mpya yameingia siku yake ya tatu hii leo huku jaji wa mahakama ya rufaa Martha Koome akiwa mwanamke wa pili kuhojiwa kwa wadhifa huo.

Akijitetea mbele ya tume ya huduma za mahakama JSC, jaji Koome ameelezea umuhimu wa kuwepo kwa haja ya mahakama ya upeo kuwa msimamo kuhusu hukumu ya kifo kwa sababu hukumu inaendelea kutolewa ilhali utafsiri wake haupo.

Jaji Koome ni mzaliwa wa mwaka 1960 kaunti ya Meru na ana uzoefu wa miaka 33 katika maswala ya kisheria tangu mwaka 1987.

Koome alijiunga na idara ya mahakama mwaka 2003 ambapo amekuwa akipanda ngazi kutoka mahakama kuu hadi mahakama ya rufaa.

Jaji Koome anahojiwa siku moja baada ya Profesa Patricia Kameri Mbote kunadi sera zake mbele ya JSC.

Jaji wa mahakama kuu Said Juma Chitembwe alifungua ukurasa wa mahojiano hayo akisema ana uwezo wa kumrithi David Maraga aliyestaafu kwa sababu ya uzoefu wake katika idara ya mahakama.

Watu 10 wameorodheshwa kuhojiwa kwa wadhifa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here