Majonzi huku Kenya ikimpoteza daktari mwingine kutokana na corona

0

Dr. Stephen Mogusu amekuwa daktari wa hivi punde kufariki kutokana na matatizo yanayoambatana na ugonjwa wa corona.

Muungano wa madaktari nchini KMPDU unasema hadi kifo chake, daktari huyo hakuwa amelipwa mshahara wake wa miezi mitano na wala hakuwa na bima ya matibabu.

Marehemu mwenye umri wa miaka Ishirini na minane alikuwa katika chumba cha watu mahututi (ICU) katika hospitali ya chuo kikuu cha Kenyatta.

Muungano wa KMPDU kupitia kaimu katibu mkuu Dr. Chibanzi Mwachonda ulikuwa unaongoza shughuli ya kuchangisha pesa kupitia kwa njia ya mtandao kwa ajili ya kusaidia katika gharama yake ya matibabu.

Daktari huyo amefariki siku moja baada ya madaktari kusitisha mgomo uliokuwa uanze Jumatatu ili kuruhusu mazungumzo baina yao na serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here