Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine ametetea handisheki baina yake na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akisema imeleta amani na udhabiti nchini.
Akizungumza katika ukumbi wa Bomas alipoongoza uzinduzi wa kampeni ya ‘Kenya Ni Mimi’, rais amesema vijana watakuwa na nafasi kubwa kupitia utekelezwaji wa ripoti hiyo na kwamba kila Mkenya atahisi kuwa anawakilishwa katika uongozi wa taifa hili.
Rais Kenyatta vile vile ametaka kukomeshwa kwa dhulma dhidi ya wanawake na wasichana katika jamii akitoa changamoto kwa machifu kuwa katika mstari wa mbele kuwaadhibu wanaohusika na uozo huo.
Akizungumza katika hafla hiyo, waziri wa habari na mawasiloano Joe Mucheru amesema miongoni mwa saini million 5.2 za BBI zilizokusanywa kwa muda wa wiki moja, zaidi ya million nne zilikuwa za vijana.
Kampeini hiyo ya‘Kenya Ni Mimi’ inalenga kuwapa vijana nafasi ya kushiriki kikamilifu katika kubuni sera zitakazowafaidi.