Maambukizi ya corona nchini yafikia 88,579

0

Watu wengine 199 wamepatwa na virusi vya corona kati ya sampuli 2,416 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii inafikisha 88,579 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.

Nairobi imerekodi visa 77, Mombasa 21, Busia 20 na Uasin Gishu 19.

Watu 485 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 69,414 huku idadi ya waliokufa ikifikia 1,571 baada ya kufariki kwa wagonjwa watano zaidi.

Walio kwenye hospitali mbalimbali ni 1,171, wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 8,127.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here