Madaktari katika hospitali za umma kaunti ya Nairobi wametangaza kuanza mgomo wao kuanzia leo baada ya mamlaka ya uongozi wa jiji NMS kukosa kutekeleza makubaliano yao ya kurejea kazini.
Katibu mkuu wa wa muungano wa madaktari KMPDU kaunti ya Nairobi Dkt. Thuranira Kaugiria amesema kuwa miongoni mwa masuala ambayo NMS chini ya jenerali Mohammed Badi wamekosa kutimiza ni kulipwa mishahara yao kwa wakati na pia kuwarejesha kazini madaktari wanne waliosimamishwa kazi.
Dkt. Kaugiria anasema wataandamana hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa kikamilifu.
Madaktari hao walitia saini mkataba wa kurejea kazini mnamo Septemba 28 na kumaliza mgomo uliokuwa umelemeza huduma katika hospitali za umma kaunti ya Nairobi.









