Padri wa Siaya sasa yuko huru

0

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji ameondoa mashtaka dhidi ya kasisi wa kanisa katoliki kaunti ya Siaya Richard Oduor aliyedaiwa kueneza virusi vya corona.

Kasisi huyo alishtakiwa katika mahakama ya Milimani na kisha kuachiliwa kwa dhamana ya Sh150,000 baada ya kukanusha mashtaka dhidi yake.

Upande wa mashtaka umeiambia mahakama kwamba umeshindwa kuwasilisha ushahidi dhidi ya padri huyo hali ambayo imesababisha kuhairishwa kwa kesi hiyo zaidi ya mara moja.

Ikumbukwe kuwa Oduor alirejea nchini kutoka jijini Roma, Italia mnamo Machi 11 na akakaa siku moja Utawala jijini Nairobi kabla ya kusafiri nyumbani kwake siku mbili baadae ambapo aliongoza mazishi ya jamaa wake wa karibu.

Baadae alirudi Nairobi na kuonyesha dalili za ugonjwa huo na kusababisha kulazwa kwake hospitalini ambapo alipimwa na kuwekwa kwenye kituo cha karantini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here