Takriban wahudumu wa afya 298 wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa wiki mbili zilizopita.
Baraza la magavana kupitia taarifa iliyotumwa na mwenyekiti wake Wycliffe Oparanya linasema wahudumu hao wanaendelea kupokea matibabu katika vituo mbalimbali vya afya.
Hata hivyo baraza hilo limeelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelea kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo katika kaunti za Nairobi na Mombasa na kuwashauri Wakenya kuzingatia masharti ya usalama kuzuia msambao huo.
Oparanya ambaye pia ni gavana wa Kakamega amesema wagonjwa 1,056 waliopatikana na corona katika kaunti 34 wangali chini ya mpango wa kushughulikiwa wakiwa nyumbani huku wengine 6,665 wakipona katika muda wa wiki mbili zilizopita.