Maandalizi yakamilika kabla ya uchaguzi wa Kiambaa na Muguga

0

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) imesema kila kitu kiko shwari kabla ya kuandaliwa kwa chaguzi ndogo za eneo bunge la Kiambaa na wadi ya Muguga Alhamisi Julai 15.

Msimamizi wa uchaguzi wa Kiambaa Peter Muigai amewaonya wawaniaji dhidi ya kujihusisha na visa vinavyokiuka sheria za uchaguzi.

Muigai amewahakikishia wapiga kura usalama wao huku akisema sheria zote za kuzuia msambao wa ugonjwa wa corona zitazingatiwa wakati wa upigaji kura.

Katika eneo bunge la Kiambaa, kivumbi ni baina ya Kariri Njama wa Jubilee na Njuguna Wanjiku wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachohusishwa na naibu rais William Ruto.

Huko Muguga, kinyanganyiro ni baina ya Kamau Thumbi wa UDA na Joseph Githinji wa Jubilee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here