Haji kupinga agizo linalozuia kushtakiwa kwa Nelson Havi

0

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji ameapa kupinga agizo la mahakama linalozuia kushtakiwa kwa rais wa chama cha mawakili nchini (LSK) Nelson Havi kuhusiana na tuhuma za kumuuzia afisa mkuu mtendaji Mercy Wambua.

Haji anasema afisi yake ilikuwa inapitia faili yenye mashtaka dhidi ya Havi baada ya kuipokea kutoka kwa idara ya upelelezi DCI kabla ya mahakama kutoa agizo la mapema kuzuia hatua zozote kuchukuliwa dhidi ya Havi.

Kutokana na hiyo, Haji amesema atapinga uamuzi huo mahakamani anaosema unakiuka katiba.

Yanajiri haya saa chache baada ya Havi kupata afueni kufuatia agizo la mahakama lililozuia kushtakiwa kwake kuhusiana na madai hayo ya kumjeruhi Wambua.

Wakati uo huo

Shirikisho la wanawake mawakili (FIDA) limemtetea Mercy Wambua kwenye mzozo baina yake na Nelson Havi.

FIDA katika taarifa wanamlaumu Havi kwa kusababisha mgogoro huo ambao umeishia kwa madai ya kuumizwa kwa Wambua.

Kupitia kwa mwenyeki wake Nancy Ikinu, FIDA wametaja kuumizwa kwa Wambua kama dhulma dhidi ya wanawake na kuwataka Polisi kuhakikisha kwamba haki imepatikana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here