MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA HIV YAONGEZEKA NCHINI

0
Viral Infection Concept.

Maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nchini yameanza kuongezeka tena, hasa miongoni mwa vijana, huku juhudi za kupunguza maambukizi hayo katika kipindi cha miaka minne iliyopita zikigonga mwamba — kutokana na changamoto za kifedha na mabadiliko ya kitabia.

Kwa mujibu wa takwimu mpya kutoka Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Maradhi ya Mlipuko (NSDCC), serikali imekuwa ikilenga kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV kwa asilimia 75 katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Hata hivyo, nchi imefaulu kupunguza kwa asilimia 60 pekee, huku maambukizi mapya yakiongezeka hasa katika kaunti za ASAL, ambapo Kaunti ya Mandera imeripoti ongezeko kubwa la asilimia 156.

Ripoti hiyo imebaini kuwa taifa linashuhudia takribani visa 6,000 vipya vya HIV kila mwaka miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24, wakati huu ambapo misaada ya wafadhili kwa sekta hiyo imepungua.

Katika tathmini ya pamoja ya mwaka ya mpango wa HIV, vifo vinavyotokana na Ukimwi kati ya mwaka 2020 na 2024 vilipungua kwa asilimia 2.5 pekee, kinyume na lengo la kupunguza kwa asilimia 50.

Mapitio ya Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Ukimwi yameonyesha kuwa ni kaunti 43 pekee zilizopunguza maambukizi mapya, kaunti tatu pekee ndizo zilizofikia lengo la asilimia 75, huku Mandera ikirekodi ongezeko kubwa zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here