SPIKA WA BUNGE LA ISIOLO AJIUZULU

0

Spika wa Bunge la Kaunti ya Isiolo, Mohamed Roba, amejiuzulu, wakati ambapo bunge hilo linakumbwa na mvutano mkali wa kisiasa kuhusu hoja ya kumng’atua madarakani Gavana Abdi Guyo.

Kupitia kwa barua kwa Karani wa Bunge la Kaunti, Roba ametaja sababu za kibinafsi kuwa msingi wa kujiuzulu kwake.

Kujiuzulu kwake kunajiri wakati wa mvutano wa kisiasa ndani ya kaunti hiyo, kufuatia mzozo mkubwa kati yake na Gavana Guyo ambaye hapo awali alikuwa mshirika wake wa karibu na pia alihusika pakubwa katika uteuzi wake kama Spika.

Roba alikuwa akiiongoza wawakilishi wadi waliokuwa wakipanga hoja ya kumng’oa Gavana Guyo, huku taarifa zikionyesha kuwa baadhi ya wawakilishi wadi walikuwa wamepiga kambi mjini Machakos kwa ajili ya maandalizi ya hatua hiyo.

Hata hivyo, mchakato huo ulisitishwa kwa agizo la mahakama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here