Maambukizi ya corona nchini yapindukia 40, 000

0

Idadi ya maambukizi ya corona nchini imepindukia 40,178 baada ya watu 271 kupatikana na virusi hivyo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amedhibitisha kuwa watu 51 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 31,710.

Watu watatu zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 751.

Nairobi inagongoza kwa kurekodi visa 81, Mombasa 58, Turkana 16, Kisumu 15, Kiambu na Garissa 13, Kisii na Machakos 10, Laikipia 8, Nandi na Nakuru 6, Kilifi, Uasin Gishu na Murang’a 5, Nyamira na Siaya 4, Kakamega, Kwale, Kajiado 2, Homabay, Mirori, Embu, Meru na Narok 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here