Baraza la Mawaziri limeidhinisha kwa kauli moja masharti makali yaliyowekwa na kamati ya usalama kutuliza joto la kisiasa nchini.
Baraza hilo chini ya uongozi wake rais Uhuru Kenyatta na kuhudhuriwa na naibu rais William Ruto limeelezea wasiwasi wake kuhusu siasa za migawanyiko ambazo zinatishia kusababisha uhasama miongoni mwa Wakenya katika siku za hivi maajuzi.
Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amepewa jukumu la kuongoza kundi litalohakikisha kuwa masharti hayo yanafuatwa.
Haya yote kwa mujibu wa mawaziri yametishia kuhujumu juhudi za serikali kuwahudumia raia wake na kuliharibia taifa hili jina katika jamii ya kimataifa.
Kwa mujibu wa baraza hilo, masharti hayo yanayojumuisha kuwafahamisha Polisi na kupata kibali siku tatu kabla ya kuandaa mikutano ya kisiasa na uchochezi wakati wa mikutano yanaanza kutekelezwa mara moja.