Ruto ahairisha mikutano yake Nyamira baada ya kutibuliwa na Polisi

0

Naibu rais William Ruto amelazimika kuhairisha ziara yake katika kaunti ya Nyamira baada ya Polisi kutibua mikutano yake miwili mapema Alhamisi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ruto amesema amefanya mashauriano na viongozi wa eneo hilo na kuafikiana kuhairisha mikutano hiyo hadi Alhamisi wiki ijayo baada ya mikutano ya leo kusambaratishwa.

Maafisa wa usalama walitumia vitoa machozi kuwafukuza vijana waliokuwa wamejitokeza kuhudhuria mkutano wa kuchangisha pesa katika shule ya msingi ya Kebirigo baada ya kukataa kuondoka kwa hiari.

Katika shule ya msingi ya Nyaangoge, hali haikuwa tofauti kwani Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya watu waliokuwa wamejitokeza kuhudhuia mkutano wa naibu rais.

Dr Ruto aliratibiwa kuzuru kaunti za Kisii na Nyamira Alhamisi na Ijumaa kuendesha michango ya makanisa mbalimbali na pia kusaidia makundi ya vijana na akina mama.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here