Maambukizi ya corona Kenya yazidi

0

Watu 551 wamepatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 4,675 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 84,169.

Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amesema kuwa watu 266 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 18,146.

Idadi ya maafa imeongezeka na kufika 1,474 baada ya watu 5 zaidi kufariki.

Wagonjwa 71 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi huku 34 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Msambao wa virusi hivi katika kaunti ni kama ifuatavyo: Nairobi 212, Kilifi 39, Mombasa 35 na Nyeri 33.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here