Madaktari washikilia kwamba mgomo wao upo kuanzia Jumatatu

0

Kuanzia Jumatatu wiki ijayo madaktari wote katika hospitali za umma wataanza mgomo wao, hii ikichochewa na hatua ya serikali kushindwa kutimiza matakwa yao.

Katibu mkuu wa muungano wa madakatri nchini KMPDU Dkt. Chibanzi Mwachonda amesema wakenya sasa wako kivyao kwani serikali imekataa kushughulikia lalama zao ikiwemo kuwapa bima ya Afya.

Mwachonda anasema licha ya kujaribu kushiriki katika mazungumzo na serikali, malalamishi yao yamekosa kutekelezwa ikiwemo kuwapa vifaa vya kujikinga wanapokuwa kazini na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Mwenyekiti wa KMPDU Dkt. Samwel Oroko anasema Wakenya wawe tayari kusalia manyumbani kuanzia Jumatatu kwani hospitali za umma zitafungwa huku akiishutumu serikali kwa kukosa kuwajali raia wake.

Itakumbukwa kwamba ilani sawa na hiyo ya mgomo imetolewa na Wauguzi pamoja na Matabibu ambao wanatazamiwa kujiunga na mgomo huo wakati ambapo taifa linapambana na janga la kimataifa la corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here