Marais Biden na Uhuru wazungumza

0

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameelezea nia yake ya kuendelea kuimarisha uhusiano mwema baina ya taifa lake na Kenya.

Biden anayeterajiwa kuapishwa rasmi mwezi ujao wa Januari baada ya kushinda uchaguzi wa urais wamezungumza kwa simu na rais Uhuru Kenyatta ambapo wamejadili maswala mbalimbali yanayohusu mataifa haya mawili.

Miongoni mwa maswala hayo ni ushirikiano utakaowezesha kushughulikia tatizo la wakimbizi, usalama na kuleta udhabiti katika kanda hii.

Rais Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wa dunia ambao wamempongeza Biden na naibu wake Kalama Harris kwa kushinda uchaguzi wa urais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here