Maafisa wa wa afya watakiwa kuondoka katika shule zilizotumika kama vituo vya karantini

0

Huku shule zikitazamiwa kufunguliwa hivi karibuni, wizara ya elimu imewataka wenzao katika wizara ya afya kuondoka na kupuliza dawa katika shule za umma zilizokuwa zinatumika kama vituo vya karantini kwa wagonjwa wa COVID19.

Katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang katika barua kwa mwenzake wa afya Susan Mochache amesema wadau wameona kwamba visa vya ugonjwa wa corona vinaendelea kupungua nchini na hivyo wameafikiana kufungua shule mapema kinyume na ilivyokuwa imekadiriwa hapo awali.

Haya yanajiri huku tume ya huduma za walimu TSC ikitoa mwongozo utakaofuatwa na walimu wanapotazamiwa kuripoti shuleni Jumatatu wiki ijayo kabla ya shule kufunguliwa.

Muhimu kwenye mwongozo huo ni kuhakikisha kuwa usafi wa madarasa pamoja na maeneo ya kulala sawa na kuwapa msaada wa kisaikolojia wanafunzi na wazazi shule zikifunguliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here