Wabunge wamkaanga Maraga

0

Hatuendi kokote maanake tulichaguliwa kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano kuwahudumia Wakenya.

Ndio kauli ya wabunge ambao wamemkaanga jaji mkuu David Maraga kwa kumshauri rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge kwa kushindwa kipitisha sheria kuhusu usawa wa jinsia.

Wabunge wakiongozwa na Junet Mohamed wa (Suna Mashariki), Otiendo Amollo wa (Rarieda) na Aden Duale wa (Garissa Mjini) wanahoji kuwa ushauri huo haufai kwani utalitumbukiza taifa katika mgogoro wa uongozi ikizingatiwa kwamba kimsingi, uchaguzi mkuu ni sharti kila baada ya miaka mitano.

Kwa mujibu wa wabunge hao, iwapo bunge litavunjiliwa mbali, ni sharti uchaguzi wa viongozi wote akiwemo rais, gavana, masenata na wawakilishi wadi uandaliwe siku moja kwa mujibu wa katiba swala ambalo ni vigumu kwa sababu tume ya uchaguzi IEBC haijabuniwa kikatiba.

Hata hivyo baadhi ya wabunge akiwemo Millie Odhiambo wa Suba Kusini wamemtetea Maraga wakisema rais anafaa kuzingatia ushauri wa jaji mkuu na kulivunja bunge.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here