Washukiwa 2 wa ubakaji washikwa Nakuru

0

Makachero wa idara ya upelelezi (DCI) wamewashika washukiwa wawili kwa kumbaka kwa awamu mwanamke mmoja katika eneo la Kuresoi Kusini, kaunti ya Nakuru.

Wawili hao Benard Korir na Nelson Langat wanadaiwa kuwa miongoni mwa genge la watu watano lililombaka kwa awamu mwanamke huyo katika kijiji cha Chigamba huko Olenguruone Septemba 19.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka Ishirini na sita baadaye alifariki kutokana na unyama huo.

Maafisa wa DCI wanasema washukiwa wengine watatu walifaulu kutoroka na bado wanatafutwa na vitengo vya usalama.

Wawili hao wanazuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani ambapo watashtakiwa kwa mauji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here